Watafiti waonya kuhusu saratani ya matiti isiyo na uvimbe

Saratani ya matiti isiyo na uvimbe Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Uvimbe wowote chini ya matiti ama maambukizi yoyote ya matiti hayanabudi kufanyiwa uchunguzi, wanasema watafiti

Karibu kisa kimoja kati ya sita vya saratani huanza na dalili nyingine tofauti na uvimbe, wataalam wanaonya.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha London wanasema kuwa wanawake wanahitaji kuelewa dalili nyingine za saratani kama vile mabadiliko ya chuchu za matiti -ili waweze kupata msaada wa haraka.

Watafiti hao walichunguza dalili za wanawake 2,300 ambao hivi karibuni waligunduliwa kuwa na saratani.

Walibaini wanawake wasiokuwa na dalili za uvimbe walikuwa walikuwa na uwezekano mkubwa wakutotembelea madaktari wao kwa uchunguzi.

Watafiri wanawasilisha kazi yao ya uchunguzi katika mkutano wa Kituo cha Kitaifa cha Taasisi ya Saratani (National Cancer Research Institute) mjini Liverpool.

Uvimbe wowote chini ya matiti ama maambukizi yoyote ya matiti hayanabudi kufanyiwa uchunguzi , walisema .

Hali kadhalika mabadiliko yoyote ya muonekano wa chuchu, kuvuja damu ama kutokwa na maji maji ya aina yoyote kwenye titi - na uvimbe wowote kwenye ngozi ya matiti.

DK. Karen Kennedy, Mkurugenzi wa Taasisi ya kitaifa ya Utafiti wa Saratani nchini Uingereza , anasema: "utafiti huu unaonyesha mara kwa mara wanawake huichelewa kwenda kumuona daktari wao kwa dalili za saratani.

" Hii inaweza kuwa ni kwasababu watu hawaelewi kuwa saratani ya matiti inaweza kujitokeza kwa njia nyingi tofauti , si tu kwa njia ya uvimbe.

" Kwa ugonjwa kama saratani ya matiti ni muhimu kubainika mapema ili mpango wa matibabu wa mapema uandaliwe na kuanza mara moja''