Shimo kubwa lameza barabara nchini Japan

Maporomoko ya barabara Fukuoka Haki miliki ya picha KYODO/REUTERS
Image caption Mporomoko huo ulianza kwa mashimo mawili madogo ambayo baadae yalianza kupanuka hadi kuwa shimo kubwa lenye kina cha mita 30m na upana wa futi 98.

Mashimo makubwa yaliyojitokeza ghafla yamemeza barabara yenye njia tano katikati mwa moja ya miji mikubwa zaidi nchini Japa Jumanne asubuhi.

Kuporomoka kwa barabara hiyo kulianza majira ya saa kumi na mbili jioni Jumatatu karibu na kituo cha treni cha Hakata , kilichopo katika mji wenye shughuli nyingi wa Fukuoka uliopo kusini mwa kisiwa cha Kyushu.

Mporomoko huo ulianza kwa mashimo mawili madogo ambayo baadaye yalianza kupanuka hadi kuwa shimo kubwa lenye kina cha mita 30m na upana wa futi 98.

Hakuna taarifa za majeruhi makubwa, lakini mifumo ya umeme, maji na gesi ilivurugika katika katika eneo hilo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shughuli za wahandisi za kupanua zaidi bara bara ya leri ya chini ya ardhi inadhaniwa kuwa na uhusiano wa mpasuko huo wa ardhi

Mtangazaji wa kituo cha habari cha NHK aliripoti kuwa mwanamke mmoja mzee aliteleza kwenye ngazi kutokana giza lililosababishwa na kukatika kwa umeme eneo hilo.

Shughuli za wahandisi za kupanua zaidi reli ya chini ya ardhi inadhaniwa kuwa na uhusiano wa mpasuko huo wa ardhi uliosababisha kutokea ghafla kwa mashimo mapana kwenye barabara, maafisa wa mji wamesema .