Mourinho awalaumu Smalling na Shaw kwa kutoshiriki mechi

Mourinho anasema wachezaji hao wangejitolea kushiriki mechi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mourinho anasema wachezaji hao wangejitolea kushiriki mechi

Kocha wa muda wa timu ya Uingereza Gareth Southgate, amewatetea wachezaji wa Manchester United Chris Smalling na Luke Shaw, baada ya wao kulaumiwa na Meneja Jose Maurinho.

Mourinho amewalaumu wachezaji hao kwa kukosa mechi ya Jamapili ambapo waliwashinda Swansea mabao 3-1 akisema kuwa wangefanya vyovyote vile kuichezea timu.

Smalling ana jeraha la mguu naye Shaw alicheza mechi la Alhamis ambapo Manchester United ilishindwa na klabu ya Fenerbahce.

Sasa Southgate anasema kuwa huenda kuna tatizo linalowakumba wachezaji hao wawili.

Smalling mwenye umri wa miaka 26 na Shaw 21, wamewachwa nje ya kikosi cha Uingereza ambacho kitashiriki mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 dhidi ya Scotland na mechi ya kirafiki ya wiki ijayo dhidi ya Uhispania.

Shaw amecheza mechi sita za ligi msimu huu tangu apone jeraha la mguu mwezi Septemba.