Besigye afanikiwa kuondoka Uganda

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Polisi wamekuwa wakiweka kuzuizi nje ya nyumba ya Besigye

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ameandika kwenye mtandao wa twitter kuwa ameondoka nchini humo licha jitihada za serikali kumzuia.

Bwana Besigye aliliambia gazeti la Daily Monitor jana kuwa, alilalimika kufuta safari yake kwenda nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne kufuatia hatua ya polisi ya kuweka kizuizi nje ya nyumba yake.

Hata hivyo msemaji wa polisi alikanusha madai hayo.

Bwana Besigye anatarajiwa kuhutubia mkutano wa tume ya kimataifa ya mawakili mjini Johannesburg siku ya Alhamis.