Watu wenye silaha washambulia treni Msumbiji

Mkataba kati ya Renamo na serikali uko kwenye hatari ya kuvunjika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkataba kati ya Renamo na serikali uko kwenye hatari ya kuvunjika

Watu wenye silaha wanaokisiwa kutoka chama kikuu ca upinzani nchini Musumbuji cha Renamo, wameshambua treni katika mkoa ulio Kaskazini mwa nchi wa Nampula.

Treni hiyo ilikuwa safarini ikielekea Nacala-a-Velha ambapo kuna bandari mpya inatuyomiwa kusafirisha makaa ya moto.

Msemaji wa polisi mkoa wa Nampula Zacarias Nacute, alimuamba mwandishi wa BBC kuwa watu hao wenye silaha waliifyatulia treni mara tatu lakini hakuna mtu alijeruhiwa.

Cha cha Renamo kimekuwa kikiendesha mashambulizi kadha dhidi ya serikali na raia katika na Kaskazini mwa Musumbiji katika jitihada za kuilazimisha serikali kuruhusu chama hicho kusimamia mikoa kinadai kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2014.