Zambia yaichapa Uganda nyumbani

Chisamba Lungu, Haki miliki ya picha Google
Image caption Mfungaji wa bao la Zambia Chisamba Lungu,

Timu ya Taifa ya Zambia almaarufu kama Chipolopolo wameibuka na Ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji wao timu ya Uganda The Cranes.

Chipolopolo walipata bao lao pekee la ushindi katika dakika ya 25 ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Chisamba Lungu,anayesakata soka la kulipwa nchini Urusi.

Ushindi wa Zambia, utawapa morali wachezaji, baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe, jumamosi iliyopita walipochapwa kwa bao 1-0.

Mchezo huu ni wa kirafiki wa kujiandaa na michezo ya kimataifa ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa komba la dunia litakalofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Uganda watacheza na Congo Brazaville, nyumbani huku Zambia, wakiwa ugenini kucheza dhidi ya Cameroon, katika kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia