Treni yashambuliwa Msumbiji

Msumbiji Haki miliki ya picha AFP
Image caption wapiganaji wa Renamo nchini Msumbiji

watu wenye silaha, wanaoshukiwa kuwa ni wanachama wa chama kikuu cha upinzania nchini Msumbiji Renamo, wameshambulia treni katika jimbo la kaskazini la Nampula.

Polisi wamesema kuwa wameshambulia kwa risasi katika treni siku ya Jumanne asubuhi.

Hakuna taarifa za majeruhi wowote wa tukio hilo.

Renamo wamekuwa na mashambulizi ya hapa na pale katika jitihada za kulazimisha serikali kuruhusu chama hiko kuongoza majimbo waliyodai wameshinda uchaguzi miaka miwili iliyopita. Renamo ilipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya serikali kwa takribani kupigana kumi na tano mwaka kiraia vita dhidi ya serikali na kumalizika mwaka 1992.