Matokeo Marekani 2016: Trump amshinda Clinton uchaguzi wa urais

Hillary Clinton and Donald Trump Haki miliki ya picha AP

Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake. Rais Obama pia amempigia simu kumpongeza na kutangaza kwamba amemwalika ikulu ya White House siku ya Alhamisi washauriane kuhusu shughuli ya mpito.

Bw Trump, aliyeeleza nia yake ya kuwafanyia kazi Wamarekani wote atakapoingia madarakani, ataapishwa kuwa rais tarehe 20 Januari mwaka 2017.

Mgombea huyo wa Republican, alishangaza wengi kwa kushinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.

Alishinda majimbo ya Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.

Bw Trump alijizolea kura 278 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

Bw Trump alishinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.

Jinsi Donald Trump alivyoshinda urais

Kisakuzi chako hakifanyi kazi na huduma hii. Lazima uwe unatumia kisakuzi cha kisasa na uwe umefungulia Javascript ndipo uweze kutazama ramani za matokeo

Chama cha Republican pia kimehifadhi wingi wa wabunge katika Bunge la Wawakilishi.

Haki miliki ya picha @realDonaldTrump / Twitter
Image caption Donald Trump alipakia picha hii kwenye Twitter, yake, mgombea mwenza wake na jamaa na marafiki wakifuatilia matokeo New York.

Kama ilivyotarajiwa, Bw Trump alishinda katika ngome za Republican katika majimbo ya Alabama, Kentucky, South Carolina, Nebraska, Indiana, West Virginia, Mississippi, Tennessee, Oklahoma na Texas, ABC News wanakadiria.

Bw Trump pia alishinda Arkansas, Kansas, North Dakota, South Dakota, Montana na Wyoming.

Bi Clinton atashinda ngome za Democratic majimbo ya New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island na District of Columbia.

Kura za Donald Trump kwenye ramani

Republican

Kisakuzi chako hakifanyi kazi na huduma hii. Lazima uwe unatumia kisakuzi cha kisasa na uwe umefungulia Javascript ndipo uweze kutazama ramani za matokeo

Mshindi alihitaji kupata kura 270 kati ya jumla ya kura 538 za wajumbe ndipo atangazwe mshindi.

Kura za Hillary Clinton kwenye ramani

Democratic

Kisakuzi chako hakifanyi kazi na huduma hii. Lazima uwe unatumia kisakuzi cha kisasa na uwe umefungulia Javascript ndipo uweze kutazama ramani za matokeo

Haki miliki ya picha Reuters

Upigaji kura ulimalizika katika majimbo 39 na matokeo kamili yalitarajiwa mwendo wa saa 23:00 EST (04:00 GMT Jumatano - Saa moja asubuhi Afrika Mashariki), upigaji kura utakaomalizika Pwani ya Magharibi. Hata hivyo yalichelewa kutokana na ushindani mkali.

Matukio mengine makuu:

  • Bodi ya Uchaguzi Carolina Kaskazini imekubali kuongeza muda wa kupiga kura maeneo manane wilaya ya Durham ambapo kuna milolongo mirefu ya wapiga kura.
  • Mgombea wa Republican aliyeshindwa kwenye mchujo Marco Rubio amehifadhi kiti chake cha useneta Florida
  • Thamani ya pesa za Mexico, peso, imeshuka sana baada ya Trump kuonekana akiongoza Florida
  • Mtu mmoja alifariki kwenye ufyatulianaji wa risasi karibu na kituo cha kupigia kura jimbo la Azusa, California. Watu watatu walijeruhiwa.

Bw Trump, tajiri kutoka Manhattan, na Bi Clinton, anayetaka kuwa rais wa kwanza mwanamke Marekani, walipiga kura mapema Jumanne katika jiji la New York.

Bw Trump alizomewa alipofika kupiga kura yake Manhattan, akiandamana na mkewe, Melania, na bintiye, Ivanka.

Wawili hao wamekuwa wakifuatilia matokeo kutoka jiji la New York.

Haki miliki ya picha @HillaryClinton / Twitter
Image caption Clinton amepakia picha hii, pamoja na ujumbe wa shukrani kwa watu wote, licha ya matokeo ya usiku wa leo

Bi Clinton atahutubia wafuasi Javits Centre, Manhattan naye Bw Trump atahutubu katika hoteli ya Hilton Midtown.

Maafisa wa polisi zaidi ya 5,000 wametumwa jijini New York kuimarisha usalama.

Utafiti wa maoni wa baada ya upigaji kura, uliofanywa na ABC News, unaonyesha wapiga kura 61% hawampendi Bw Trump nao 54% ndio hawampendi Bi Clinton.

Mapema Jumanne, Bw Trump kwa mara nyingine alikataa kusema iwapo angekubali matokeo.

"Tutaangalia tuone vile mambo yatakuwa," aliambia Fox News, huku akidai kwamba kumekuwa na kasoro hapa na pale kwenye uchaguzi.

"Ninataka kila kitu kiwe wazi."

Katika baadhi ya vituo, mitambo ya kupigia kura ilifeli na kwingine kukawa na milolongo mirefu, lakini yalionekana kuwa matatizo ya kawaida.

Bw Trump, aliyezua utata kuhusu kuaminika kwa shughuli ya uchaguzi kwa kudai kura "zitaibwa" mapema, pia amewasilisha kesi ya dharura Nevada.

Maafisa wa Republican walimshtaki msajili wa wapiga kura wilaya ya Clark, wakidai jimbo hilo lilifungua vituo vya kupigia kura muda mrefu kuliko inavyofaa.

Lakini jaji ameitupilia mbali kesi hiyo.

Kando na kura za urais, Wamarekani wamekuwa pia wakipiga kura za Maseneta, wabunge wa Bunge la Wawakilishi na Magavana.

Viti vyote 435 Bunge la Wawakilishi vilikuwa vinashindaniwa, na ABC News wanakadiria kwamba bunge hilo litabaki chini ya udhibiti wa Republican.

Lakini theluthi moja ya viti Seneti, ambao Republican wamekuwa wanaongoza, pia vinashindaniwa, na Democratic wanatumai wanaweza kudhibiti bunge hilo.

Jumla ya Wamarekani 45 milioni, idadi kubwa zaidi kuliko awali, walijitokeza kupiga kura mapema.

Bw Trump na Bi Clinton walikuwa wanapigania kumrithi Barack Obama wa Democratic.

Rais Obama haruhusiwi kuwania kikatiba baada ya kuhudumu mihula miwili ya miaka minne.

Rais mpya ataapishwa tarehe 20 Januari 2017.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii