Matokeo ya uchaguzi Marekani yayumbisha hisa Asia

vibonzo vya Hillary Clinton na Donald Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Viwango vya hisa katika masoko yote makuu ya hisa barani Asia kwa sasa vimeporomoka

Masoko ya hisa ya Asia yameyumba baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa Marekani kuonyesha ushindi wa Donald Trump kuwa ya kuaminika.

Thamani ya dola ya Marekani pia imeshuka.

Viwango vya hisa katika Masoko yote makuu katika kanda hiyo ya Asia kwa sasa vimeshuka, huku pesa zikielekezwa katika hisa salama, dhahabu na sarafu ya Japan- yen.

Wakati huo huo sarafu ya Mexico -Peso imeporomoka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa dhidi ya dola.

Kwa kiwango ambacho wafanyabiashara walitarajia ushindi wa moja kwa moja wa Hillary Clinton, hata mchuano mkali pekee unatosha kuyumbisha sarafu hiyo.

Wastani wa viwango vya hisa nchini Japan Nikkei 225 uko chini kwa 2.2% kuku lile la Hang Seng la mjini Hong Kong likishuka kwa 3.5% , hali kadhalika Shanghai pia limeshuka kwa 1.3%.