California yaidhinisha matumizi ya bangi kwa kujifurahisha

Ukulima wa bangi California Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Bangi iliyohalalishwa kisheria kwa matumizi ya dawa katika jimbo la California, sasa itatumiwa kwa kujifurahisha

.

Wapiga kura katika majimbo ya California na Massachusetts wameidhinisha matumizi ya bangi(marijuana) kwa kura.

Kura ya kuidhinisha matumizi ya mmea huo iliyopigwa sambamba na ile ya uchaguzi wa rais, inaidhinisha kisheria uzalishaji na matumizi ya bangi kwa watu wenye umri wa miaka 21.

Wapigaji kura katika majimbo mengine waliopigia kura kuidhinisha kwa matumizi ya bangi kwa ajili ya kujifurahisha ni Arizona, Maine, na Nevada, ambako matokeo bado hayajajulikana.

Watu katika majimbo ya Florida na North Dakota, wakati huo huo, waliithinisha kisheria mmea wa bangi kwa matumizi ya tiba.

California ilisema ushuru juu ya mauzo na kilimo cha bangi utasaidia kuboresha mipango ya vijana, mazingira na utekelezwaji wa sheria.

Wanaopinga matumizi ya bangi hata hivyo yanatoa fursa kutolewa kunadiwa kwa matumizi ya muhadarati huo kwenye vipindi vya televisheni vinavyoangaliwa na vijana wao, suala litakalochochea "kuharibu afya na usalama'' .

Katika Massachusetts, sheria hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa mwenzi Disemba, huku hatua sawa za matumizi ya ushuru utokanao na bangi zikiwa sawa na zile za jimbo la California.

California lilikuwa ni moja ya majimbo ya kwanza kupitisha sheria ya bangu kwa matumizi ya kitabibu mnamo mwaka 1996.

Jumanne , wapiga kura wa Florida na North Dakota walifuata mkumbo huo huo kwa kuidhinisha kwa wingi wa kura kwa matumizi ya dawa.

Majimbo mengi nchini Marekani yametumia uchaguzi mkuu kama fursa ya kuweka kwenye mzani maswali kwa umma kuhusu masuala kama ushuru, kima cha chini cha mshahara ama hukumu ya kifo.

Nebraska imeidhinisha kwa mara nyingine tena hukumu ya kifo

Ingawa jimbo hilo halijawahi kutekeleza hukumu ya kifo kwa mfungwa yeyote tangu 1997, lina watu 10 walioorodheshwa kuawa

Wakati huo huo wapiga kura wa Colorado waliidhinisha kifo cha kusaidiwa kwa wagonjwa mahututi kupitia "dawa ambayo mtu anaweza kujichagulia mwenyewe ".