Ahadi za Trump ndani ya siku 100 za kwanza madarakani

Trump ameahidi kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump ameahidi kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico

Ni kipi Donald Trump ameahidi kukifanya siku za kwanza 100 akiwa rais?

Hakujakuwa na mgombea wa urais katika historia ya Marekani kama mfanyabiashara tajiri Donald Trump.

Matamshi yake yenye utata na msimamo mkali kuhusu uhamiaji, vilileta msukosuko ndani ya chama chake na mgawanyiko nchini.

Lakini ahadi yake ya "kuiweka mbele nchi "iliwavutia mamilioni ya waamerika ambao wanahisi kuhujumiwa na mfumo wa sasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump ameahidi kuboresha uhusiano na rais wa Urusi Vladimir Putin

Kwa hivyo ni kipi tunatarajia kutoka kwa bwana Trump?

Baadhi ya ahadi zake ndani ya siku 100 za kwanza zilitolewa wakati wa hotuba yake mwezi uliopita mjini Gettysburg jimbo la Pennsylvania.

Ameapa kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, mradi ambao utagharamiwa na Mexico.

Ahadi nyingine ambayo licha ya kutokuwepo kwenye hotuba ya Gettysburg ni kusaini upya mikataba ya biashara kati Marekani,Canada na Mexico.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ameapa kusaini upya mikataba ya biashara kati ya Marekani, Canada na Mexico

Anasema kuwa mikataba hii inachangia katika kuwapokonya raia ajira zao.

Trump pia ameahidi kuboresha uhusiano na Raias wa Urusi Vladimir Putin, ambaye amemsifu na kumtaja kuwa kiongozi aliye imara.

Aidha ameapa kuondoa Marekani kutoka kwa mkataba kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.