Jinsi kuchaguliwa kwa Trump kutaibadilisha dunia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Athari ya kuchaguliwa kwa Trump duniani

Ushindi wa Donald Trump kama rais wa Marekani utabadilisha uhusiano wa Marekani na dunia nzima katika njia tofauti.

Haki miliki ya picha APA
Image caption Mawaziri wa ulinzi wa nchi za NATO

Trump amekuwa akilikosoa shirika la kujihami la nchi za Magharibi NATO, ambayo ni nguzo ya sera za kigeni za Marekani kwa zaidi ya miaka 60.

Amelitaja shirika hilo kuwa lisilo la maana na kuwaelezea wanachama wake kama wasio na shukran ambao hunufaika kutoka Marekani. Ametisha kuwa ataondoa vikosi vya Marekani ikiwa hawatalipa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Trump anataka kuboresha uhusiano na Putin

Upande wa Urusi, Trump amesema kuwa anaamini kuwa anaweza kutuliza misukosuko na rais Vladimir Putin na amemsifu kuwa kiongozi aliye imara ambaye angependa kuwa na uhusiano naye.

Tangu Obama aingie madarakani uhusiano kati ya Urusi na Marekani umekuwa mbaya hadi kufikia hatua ambapo nchi hizo zinaunga mkono pande tofauti nchini Syria.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Trump: Mkataba nuklia na Iran ulikuwa mbaya zaidi

Kwa Rais Obama, makubaliano ambapo Iran iliondolewa vikwazo ili iachane na mipango ya nuklia, ilikuw ni historia kwa Marekani.

Lakini Donald Trump ameyataja kuwa makubaliano mabaya zaidi. Amesema kuwa kuuavunja makubaliano hayo itakuwa ajenda yake kuu.

Barani Asia kuchaguliwa kwa Trump kunaibua maswali mengi ya kiusalama. Japan na Korea Kusini zimetajwa na Trump kama zinaoitegema sana Marekani.

Hata amenukuliwa akisema kuwa zinaweza kunufaika kwa kuwa na silaha zao za kinyuklia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump atakabiliana vipi na jamaa huyu- Kim Jong-un

Pia kuna nchi inaitwa Korea Kaskazini ambayo kwa sasa inatengeneza zana za kinyuklia. Trump anakabiliwa na kibarua cha kuzima mipango hiyo, kitu ambacho kimewashinda viongozi wa awali wa Marekani.