Hillary Clinton: Trump apewe fursa ya kuongoza

Hillary Clinton akubali matokeo Haki miliki ya picha AFT
Image caption Hillary Clinton akubali matokeo

Mgombea wa urais aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa rais mteule Donald Trump anafaa kupewa nafasi ili kuongoza.

Akionekana kwa mara ya kwanza tangu kukiri kushindwa ,mgombea huyo wa chama cha Democrat amesema kuwa ana matumaini kwamba Trump atafanikiwa kuwa rais wa Wamarekani wote.

''Tumeona kwamba taifa letu limegawanyika sana zaidi ya nilivyodhania'',alisema bi Clinton.

Donald Trump atakuwa rais wa 45 wa Marekani baada ya ushindi mkubwa.

Atafanya mkutano wake wa kwanza wa mpito na rais Obama katika ikulu ya White House siku ya Alhamisi.

Bwana Obama alimpongeza mrithi wake katika mazungumzo ya simu mapema asubuhi akisema kwamba sio siri kwamba yeye na Trump wana tofauti kubwa kati yao.

Image caption Wafuasi wa Clinton wakionyesha hisia zao wakati mgombea huyo aliyeshindwa alipokuwa akitoa hotuba yake

''Hatahivyo tuko katika timu moja na watu wanafaa kujua kwamba sisi ni Wamarekani kwanza tunataka taifa hili kuboreka zaidi''.

Bi Clinton aliwaambia wafuasi wake akitaja kushindwa kwake katika uchaguzi huo katika hotubu yake huko New York.

''Bado hatujaafikia lengo letu .Lakini siku moja mtu ataafikia'', alisema Bi Clinton.

''Kwa wasichana wote wanaotazama hotuba hii...ondoeni shaka kwamba muna thamani tele na uwezo mkubwa na munapaswa kupewa kila fursa duniani'',alisema. Nawapa pole kwamba hatukushinda kutokana na thamani tulio nayo kati yetu na maono yetu tulionayo kwa taifa hili''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii