TB Joshua aondoa utabiri wa ushindi wa Clinton Facebook

Walioshangazwa na hatua ya TB Joshua Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Walioshangazwa na hatua ya TB Joshua

Utabiri uliofanywa na muhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua kwmba Hillary Clinton atashinda uchaguuzi wa urais nchini Marekani umeondolewa katika akaunti yake ya facebook.

Bwana Joshua aliwaambia wafuasi wake siku ya Ijumaa kwamba ameona mwanamke akishinda.

Baada ya Donald Trump kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa Jumanne ,wageni katika ukurasa wa facebook wa Muhubiri huyo walishangaa walipoona utabiri huo umeondolewa.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Walioshangazwa na hatua ya TB Joshua

Muhubiri huyo tajiri anajulikana kama 'mtume' na wafuasi wake.

Ni mmojawapo wa wahubiri maarufu nchini Nigeria na anajulikana sana barani Afrika huku wanasiasa wengi wakiwa wafuasi wake.