Kura za maoni zashindwa kutabiri ushindi wa Trump

Kampuni za kura ya maoni zafeli kutabiri ushindi wa Trump
Image caption Kampuni za kura ya maoni zafeli kutabiri ushindi wa Trump

Kampuni za kura ya maoni nchini Marekani zilishindwa kutabiri ushindi wa Bw. Trump katika kile wachanganuzi wanasema ni pigo kubwa kwa sekta hiyo.

Kulikuwa na tatizo kama hilo mnamo mwezi Juni nchini Uingereza ambapo kambi ya watu waliotaka kujiondoa kwa Uingereza katika muungano wa Ulaya hawakuonekana kuwa tishio.

Kura ya maoni ya hivi karibuni ilionyesha kuwa bi. Clinton alikuwa anaongoza kwa asilimia 4 na ilionekana kwamba watu wengi walimuunga mkono Clinton ikilinganishwa na rais mteule Donald Trump,huku ikiwa hakuna hata kampuni moja ya kura hizo za maoni iliotabiri ushindi wa Trump.