Wanajeshi wa Urusi waitimua manuwari ya NATO

Manuwari ya NATO yafukuzwa na wanajeshi wa Urusi kwa kufanya upelelezi
Image caption Manuwari ya NATO yafukuzwa na wanajeshi wa Urusi kwa kufanya upelelezi

Wizara ya ulinzi nchini Urusi inasema kuwa jeshi lake la wanamaji limeifukuza manuwari moja ya kijeshi ya taifa la Uholanzi .

Msemaji wake meja jenerali Igor Konashenkov ,alisema kuwa manuwari hiyo ya NATO ilikuwa na utaratibu mbaya na hatari ambao huenda ungesababisha ajali kubwa.

Msemaji huyo amesema kuwa msafara wa jeshi la Urusi uliigundua manuwari hiyo ambayo ilikuwa ikichunguza mwenendo wa wanajeshi hao ,ikiwemo meli moja ya Marekani.

Amesema kuwa manuwari kama hizo hazifai kufanya uchunguzi kutokana na uwezo wake wa kupiga maji mingi.