Lukaku kuondoka Everton msimu ujao

lukaku Haki miliki ya picha Google
Image caption Romelu Lukaku akiwa na kocha wake Ronald Koeman

Meneja wa Everton Ronald Koeman anaamini mshambuliaji wake Romelu Lukaku ataondoka klabuni hapo msimu ujao na kwenda anakostahili kuonesha kipaji chake.

Koeman anaamini, mchezaji huyo anao uwezo wa kuichezea klabu kubwa kama FC Barcelona ambayo ndio inasifika kwa bora duniani.

Mwanzoni mwa Msimu huu, Lukaku aliomba kuhama Everton lakini akabembelezwa na kukubali kusalia klabuni hapo kwa Msimu mmoja.

Koeman ameeleza: "Nilimwezesha kujiamini na mwenyewe ametambua ni safi kwake kubaki Everton kwa Msimu mmoja ili ajiendeleze zaidi."

Koeman anamfananisha nyota wake huyo na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na Barcelona Patrick Kluivert.

Romelu Lukaku alijiunga na Everton kwa Mkopo kutoka Chelsea Mwaka 2013 na kisha kusaini mkataba wa kudumu mwaka 2014.