Yanga dimbani kuwakabili Ruvu Shooting

Yanga Haki miliki ya picha Google
Image caption Kikosi cha timu ya Yanga

Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya Yanga almaarufu kama timu ya wanainchi watakua wenyeji wa Ruvu Shooting.

Vinara wa ligi hiyo Simba walipoteza mchezo jana huko mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prison kwa mabao 2-1 na kuwa mchezo wao wa pili kupoteza.

Azam FC wao wakicheza ugenini Mkoani Shinyanga walishinda kwa ushindi mnene wa mabao 4-1 dhidi ya Mwadui.

Msimamo wa ligi ulivyo Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 35, wakiwa wamecheza michezo 15, Yanga wako nafasi ya pili kwa alama 30 wakiwa wamecheza michezo 14.

Azam ana alama 25 nafasi ya tatu huku wakiwa wamecheza michezo 15. Kagera Sugar wana alama 24 kwa michezoi 15 wako nafasi ya nne.