Amnesty: Polisi wanakiuka haki za binadamu Iraq

Mosul Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zaidi ya watu 40,000 wamepoteza makazi yao ndani ya wiki tatu ziliopita huko Mosul

Kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa serikali ya Iraq kuchunguza ripoti juu ya polisi kuwatesa na kuwaua raia katika vijiji Kusini mwa Mosul.

Kikundi cha watafiti walikwenda katika eneo hilo baada ya vikosi vya Iraq kufukuza wanamgambo wa Islamic state mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mashahidi walisema kuwa takribani watu sita wamepigwa risasi na watu waliovalia sare za polisi. . Mwakilishi Amnesty huko Beirut, Lynn Maalouf, amesema kuwa yeyote anaetuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita lazima aadhibiwe, wakisubiri uchunguzi wa kimahakama.

Mada zinazohusiana