Uchunguzi dhidi ya Brad Pitt wasitishwa

Brad Pitt na Angelina Jolie Haki miliki ya picha AP
Image caption Pitt anataka kupata haki sawa ya kuwatunza watoto wake na Jolie

Uchunguzi wa madai kwamba Brad Pitt amekuwa na tabia ya ukatili dhidi ya mwanawe wa kiume umesitishwa, vyombo vya habari Marekani vimeripoti.

Maafisa wa huduma kwa jamii mjini Los Angeles wamekuwa wakichunguza madai kwamba Bw Pitt alimgonga Maddox, 15, wakiwa kwenye ndege ya kibinafsi.

Mkewe Angelina Jolie aliwasilisha ombi la talaka siku ambayo kisa hicho kilitokea.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya mwongo mmojja.

Bw Pitt sasa anapigania kupata haki sawa ya kukaa na watoto wao sita.

Msemaji wa Idara ya Huduma za Familia ya Watoto LA amesema idara hiyo haiwezi kuthibitisha iwapo maafisa wake walimchunguza itt.

Bi Jolie alitaja "tofauti zisizoweza kusuluhishwa" kama sababu yake kuwasilisha ombi la kutaka kuvunja ndoa yao 19 Septemba.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Brad na Angelina wakiwa na watoto wao Novemba 2011

Bw Pitt na Bi Jolie walianza urafiki wakiandaa filamu ya 2005 kwa jina Mr & Mrs Smith, ambapo waliigiza wachumba walio kwenye uhusiano uliokwama. Walioana 2014.

Ndoa hiyo ilikuwa ya pili kwa Pitt, baada yake kutaliniana na nyota mwigizaji wa kipindi cha Friends, Jennifer Aniston.

Kwa Bi Jolie ilikuwa ya tatu baada ya ndoa zake kwa Billy Bob Thornton na Jonny Lee Miller.

Wana watoto sita - Maddox, Pax, na Zahara, ambao ni wa kupangwa, na wa kuzaliwa Shiloh na pacha Knox na Vivienne.

Bw Pitt, 52, na Bi Jolie, 41, walifunga ndoa kwenye sherehe ya harusi ya faraghani eneo la Provence, Ufaransa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii