Uchaguzi Marekani 2016: Michelle Obama mwaka 2020?

Bi Obama ni maarufu sana katika siasa za Marekani kwa sasa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bi Obama ni maarufu sana katika siasa za Marekani kwa sasa

Nani ameanza kufikiria kuhusu uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani? Kunaye?

Naam, ingawa si wengi, kunao walioanza kufikiria kuhusu uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani, sana wengi waliokuwa wanamuunga mkono Bi Hillary Clinton wa chama cha Democratic aliyeshindwa na Donald Trump wa Republican.

Uchaguzi mkuu hufanyika kila baada ya miaka minne, maana kwamba wanafikiria kuhusu Novemba 2020.

Aliyeanza kuzungumziwa sana ni mke wa Rais Obama, Michelle Obama, ambaye kando na kuwa mwanamke kama Bi Clinton, ameonyesha kuwa na sifa nzuri.

Ni mmoja wa waliotia juhudi sana siku za mwisho za kampeni upande wa Bi Clinton na alimshambulia sana Bw Trump.

Marekani kwa sasa ni taifa lililogawanyika kisiasa, lakini umaarufu wake unaonekana kuvuka mipaka.

Mamia tayari walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya ushindi wa Trump kumhumiza Michelle awanie 2020.

"Mazingira mwafaka sana kwa Michelle Obama kushinda uchaguzi 2020," mmoja aliandika.

Mwingine alisema: "Michelle Obama 2020 tafadhali Michelle Obama 2020 tafadhali Michelle Obama 2020 tafadhali".

Kwa mujibu wa utafiti wa Gallup, Bi Obama anapendwa asilimia 64 na Wamarekani, kiwango kilicho juu ya Donald Trump, Hillary Clinton na hata mumewe.

Kuna tatizo moja hata hivyo, kwani Bi Obama mapema mwezi Machi alisema hana nia ya kuwania urais.

Lakini hata hivyo mambo mengi yamebadilika tangu wakati huo.

Bi Clinton, wakati wa hotuba yake baada ya kushindwa, alisema ingawa mwenyewe hakufanikiwa, anaamini siku sijazo kutakuwepo mwanamke atakayefanikiwa.

Haki miliki ya picha @Melusine78
Haki miliki ya picha llSuperwomanll

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii