Kutana na wale wanaotarajiwa kuwa mawaziri wa Trump

Hili huenda likawa baraza la mawaziri la Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hili huenda likawa baraza la mawaziri la Trump

Kwa sasa kilicho kwenye akili za wengi ni kuhusu nani watapewa nyadhifa za juu kwenye uongozi wa rais aliyechaguliwa nchini Marekani Donald Trump.

Wakati wa hotuba yake ya ushindi, Trump aliwasifu wale waliosimama naye ambao mara nyinyi wanaonekana kuwa wanaosubiri kujiunga kwenye baraza lake la mawaziri

Wasaidizi wake walikuwa tayari walikuwa wamesambaza majina ya watu ambao walionekana kuwa bora kwa baraza la mawaziri siku za mwisho mwisho za kinyanganyiro cha kuwania urais

Hawa ni baadhi ya wale ambao wanaonekana kuwa huenda wakajiunga na baraza hilo.

Huwezi kusikiliza tena
Je huenda hili likawa baraza la mawaziri la Trump?

Newt Gingrich - Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni

Alikuwa mfuasi wa Trump ambaye aliingia kwenye orodha ya wale waliotarajiwa kuwa wagombea wenza wa Trump, na ametajwa kuwa mwanadiplomasia wa hadhi ya juu nchini Marekani

Alikuwa spika wa bunge la wawakilishi mwaka 1994.

Gingrich mwenye umri wa amiak 73 alishindwa wakati alijaribu kuwania uteusi wa kuwa mgombea urais wa Republican mwaka 2011.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Newt Gingrich

Rudy Giuliani - Mwanasheria mkuu

Ni mmoja wa wafuasi sugu wa bwana Trump. Anatajwa kuwa mtu anayeweza kupewa wadhifa wa mwanasheria mkuu nchini Marekani.

Akiwa meya wa mji wa New York wakati wa shambulizi la Septemba mwaka 2011, alipata umaarufu mkubwa wakati huo.

Giuliani ashahudumu kama mkuu wa mashtaka wa jimbo la New York. Pia aliwania uteuzi wa urais wa chama cha Republican mwaka 2008, lakini akajiondoa baada ya kushindwa na John McCain na Mitt Romney wakati wa mchujo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rudy Giuliani

Reince Priebus - Mkuu wa watumishi wa Rais

Bwana Priebus mwenye umri wa miaka 44 anaonekana kuwa mtu anayeweza kupewa wadhifa wa kusimamia masuala ya ikulu

Ni rafiki wa karibu wa spika Paul Ryan, ambaye anaonekana kuwa muhimu katika kutekeleza masuala ya ungozi wa serikali mya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Reince Priebus

Chris Christie - Waziri wa biashara

Baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania urais mwaka huu, gavana huyo wa New Jersey alimuunga mkono bwana Trump

Bwana Christie mwenye umri miaka 54 ametajwa kwa nyadhifa tofauti ikiwemo ya waziri wa biashara.

Lakini amekumbwa na kashfa inayohusu kufunga kwa daraja linalounganisha majimbo la New Jersey na New York kwa madai ya kumuadhibu meya wa eneo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chris Christie

Jeff Sessions - Waziri wa ulinzi

Ni seneta kutoka Alabama ambaye anatajwa kuwa anayeweza kuwa mkuu wa ulinzi.

Trump alimsifu Sessions wakati wa sherehe ya ushindi mjini New York.

Sessions mwenye umri wa miaka 69 aliunga mkono uvamizi nchini Iraq mwaka 2003.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeff Sessions

Michael Flynn - Mshauri wa masuala ya ulinzi

Bwana Flynn ni mwanajeshi mstaafu ambaye alimsaida Trump, kuwafikia wanajeshi wastaafu licha ya Trump kutohudumu katika jeshi.

Anasema alilazimishwa kuacha wadhifa wake kama mkurugenzi wa ujasusi kati ya mwaka 2012 na 2014 kutokana na maoni yake kuhusu siasa kali za kiislamu.

Wakati wa kampeni alikosoa sera za utawala wa Rais Obama dhidi ya kundi la Islamic State.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Michael Flynn

Steven Mnuchin - Waziri wa fedha

Trump mwenyewe amemtaja mwenyekiti wa masuala yake ya fedha kwa wadhifa wa waziri wa fedha.

Mr Mnuchin alipata utajiri wake katika kipindi cha miaka 17 alihudu katika kampuni ya Goldman, kabla ya kuanzisha kampuni yake ya filamu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Steven Mnuchin