Obama na Trump kukutana White House leo

Haki miliki ya picha OTHER
Image caption Obama na Trump kukutana White House leo

Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajianda kuelekea Ikulu ya White House kuanza mazungumzo na Rais Barack Obama, kuhusu kupokezana madaraka. Trump ataandamana na mkewe Melania ambaye atakutana na michelle Obama.

Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano aliishauri timu yake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna mafanikio kwenye shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi Januari.

Mapema timu ya kampeni ya Trump ilikutana na washauri kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi muhimu katika nyadhifa za serikali.

Majina yaliyotajwa ni kati ya wale waliomuunga mkono Trump kutoka mwanzo akiwemo aliyekuwa spika Newt Gingrich, maseneta Jeff Sessions na Bob Corker pamoja na aliyekuwa meya wa New York Rudy Giuliani.