Trump alikuwa akiwasiliana na Urusi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Urusi Vladimir Putin

Maafisa nchini Urusi wanasema kuwa walikuwa kwenye mazungumzo na timu ya kampeni ya Trump siku za kuelekea kwenye uchaguzi

Trump amekuwa akikana madai ya kuwa na mawasiliano na serikali ya Urusi lakini naibu waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi Sergei Ryabkov, aliliambia shirika la habari la serikali kuwa kulikuwa na mawasiliano.

Wale watu ambao wamekuwa kwenye msitari wa mbele walio katika nyadhifa za juu, wachache wamekuwa kweny mawasiliano na waakilishi wa Urusi, alisema Rybakov.

Msemaji wa Trump Hope Hicks, alisema kuwa hakukuwa na mawasiliano yoyote kati ya Urusi na timu yaTrump kabla ya Jumanne.