Barton na Rangers wakubaliana kuvunja mkataba

Barton Haki miliki ya picha Google
Image caption Joey Barton

Mchezaji raia wa Uingereza Joey Barton, amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu yake ya Rangers, inayoshiriki ligi kuu ya nchini Scotland.

Barton mwenye umri wa miaka 34, mkataba wake ulikua unamalizika mwaka 2018, na ameichezea Rangers michezo nane toka ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Burnley, mwezi Mei mwaka huu.

Mchezaji huyu alifungiwa kwa muda wa wiki sita na timu yake baada kutokea mabishanao katika zoezi mwezi Septemba, pia amekua akichunguzwa na chama cha soka cha Scotland kwa tuhuma za kukiuka sheria na uchezaji Kamari.

Nyota huyu wa zamani wa vilabu vya Manchester City, Newcastle, Marseille na QPR player, amewashukuru mashabiki wa Ranger, na kuitakia timu hiyo mafaniko.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Ujumbe wa Joey Barton katika ukurasa wake wa mtandao wa Twita