Argentina hoi kwa Brazil yachapwa 3-0

Brazil Haki miliki ya picha AP
Image caption Washambuliaji wa Brazil wakishangilia kwa staili ya kupiga simu

Michezo mitano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mwaka 2018, imecheza kwa ukanda wa Marekani Kusini.

Brazil wakicheza katika dimba la Belo Horizonte, wamewachapa Argentina kwa mabao 3-0, mabao ya brazili yakifungwa na Philipe Couthino, Neymer, na Paulinho.

Venezuela wakicheza nyumbani nao wameibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwachapa bolivia kwa mabao 5-0.

Paraguay wamekubali kichapo nyumbani baada ya kufungwa mabao 4-1 na Peru,Uruguay wakashinda kwa mabao 2 - 1 dhidi ya Ecuador

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mfungaji wa bao la kwanza la Uruguay Sebastian Coates akishangilia na Diego Godín

Colombia wakashindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoshana nguvu na Chile kwa sare ya bila kufungana.