Trump aeleza vipaumbele vya sera zake

Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Baada ya mkutano na msemaji wa Republican Paulo Ryan, rais mteule wa Marekani Bwana Donald Trump ameeleza vipaumbele vya sera zake.

Mteule huyo amesema atapunguza kodi na kufanya mageuzi ya sekta ya huduma za afya kwa kuachana na mfumo uliowekwa na Barack Obama.

Pia amesema atabadili haraka sheria juu ya uhamiaji , Hizo ni miongoni mwa hatua tatu muhimu alizoahidi kwenye kampeni zake za Urais.

Alisema yeye atafanya mambo ya kuvutia kwa ajili ya watu wa Marekani. Lakini baadhi ya ahadi alizotoa kwenye kampeni zimeondolewa kwenye tovuti yake ikiwemo tishio la kupiga marufuku Waislamu kuingia Marekani, kuachana na makubaliano ya Paris katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kampeni za Trump zisingeweza kusema kuhusu mabadiliko hayo ya tovuti.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii