Umoja wa Mataifa: Kuna upungufu mkubwa wa chakula Aleppo

Jan Egeland
Image caption Mratibu wa masuala ya kibadamu Jan Egeland

Umoja wa Mataifa umesema kuwa hifadhi ya chakula ya mwisho imeweza kusambazwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi huko Mashariki mwa Aleppo.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu, Jan Egeland, amesema kuwa hakutakua na chakula cha kusambaza wiki ijayo labda umoja wa mataifa wasambaze upya.

Bwana Egeland ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa ulikuwa ametoa mpango wa kina kwa ajili ya kutoa misaada mashariki mwa Aleppo lakini kutokana na masharti ya mara kwa mara imekua vigumu kutoa misaada.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Eneo la mji wa Aleppo

Umoja wa Mataifa umedai kufanyike usitishwaji wa mapigano zaidi ya saa kumi zilizopendekezwa na Urusi.

Wakati huo huo Wizara ya Ulinzi ya Urusi imekosoa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutumia fursa ya kutoa misaada.

Mada zinazohusiana