Mwindaji aliyeua Simba aondolewa mashtaka Zimbabwe

Haki miliki ya picha PAULA FRENCH
Image caption Cecil

Mahakama nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi dhdi ya muwindaji Theo Bronkhurst, inayohusu mauaji ya simba kwa Jina Cecil aliyeuawa mwaka 2015.

Simba huyo aliuawa na daktari raia wa Marekani mwezi Julai mwaka 2015, kisa ambacho kilishutumiwa kote dunaini.

Simba huyo wa umri wa miaka 13 amekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kwenye mbuga ya kitaifa ya Hwange nchini Zimbabwe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Theo Bronkhurst analaumiwa kwa kushindwa kuzui mauaji ya simba Cecil

Zimbabwe ilimlaumu Theo Bronkhurst kwa kumhadaa Cecil kutoka nje ya mbuga hiyo, na kisha kuuawa na mwindaji akitumia mshale.

Cecil alikuwa amewekewa kifaa cha kumfuatilia cha GPS kwa utafiti na chuo cha Uingereza cha Oxford.

Mauaji ya Cecil yalisababisha kuanza kwa kampeni ya kimataifa ya kumaliza uwindaji wa Simba.