Uongozi wa Trump: Maswali na majibu

Trump

Chanzo cha picha, AP

Kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa rais mteule wa Marekani pamoja na chama chake kuchukua udhibiti wa bunge la Congress, kumezua maswali chungu nzima kuhusu uchaguzi huo na ni kipi kitafuatia.

Kuanzia bima ya afya, ndoa za jinsia moja, mabadiliko ya hali ya hewa na Obamacare. Raia wa Marekani kote duniani wanataka kujua hali ya siku zao za baadaye chini ya uongozi mpya. Haya ni baadhi ya maswali yanayoulizwa kwenye mitandao

Ni watu wangapi walipiga kura kwenye uchaguzi wa Marekani?

Maafisa wa uchaguzi hawatakuwa wamejumuisha takwimu zote hadi muda wa wiki mbili tangu siku ya upigaji kura. Lakini takwimu za kwanza zinaonyesha kuwa watu milioni 128.8 walipiga kura kati ya wapiga kura milioni 231.5 waliosajiliwa, ambayo ni asilimia 55.6.

Ni nani alipata kura nyingi zaidi?

Hillary Clinton anaonekana kupata kura nyingi lakini tofauti kati yao ni ndogo.

Hesabu zinaonyesha kuwa Bi Clinton alishinda kura 60,274,974 ambayo ni asilimia 47.7 ikilinganishwa na Donald Trump ambaye alipata kura 59,937,338 ambayo ni asilimia 47.4.

Chanzo cha picha, EPA

Hata hiyo mfumo ambao hutumiwa kumchagua rais nchini Marekani unasema kuwa wagombea ni lazima washinde kura za wajumbe, yaani "Electoral College". Kutokana na hilo ushindi wa Trump kwenye majimbo yenye kura nyingi za wajumbe ulimzolea kura 290. Matokeo ya majimbo mawili ya Michigan na New Hampshire bado hayajatangazwa.

Wagombea walikuwa na umri gani?

Kujibu moja ya maswali yanayoulizwa zaidi mitandaoni- Donald Trump ana miaka 70 naye Hillary Clinton ana miaka 69.

Trump ataingia lini rasmi uongozini?

Ataapishwa siku ya Ijumaa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 2017. Lakini kabla ya siku hiyo atatangaza timu yake, apewe taarifa za siri zikiwemo za siri, kuhusu usalama na oparesheni za kijeshi.

Trump ataishi ikulu ya White House?

Wakati wa mahojiano na mtandao moja mwaka uliopita, bwa Trump alionekana kuzima uvumi kuwa atakiuka tamaduni ya miaka mingi ya kuishi ikulu na hata mjini Washingto

Kwenye mahojiano hayo Trump alisema kuwa bila shaka ataishi kwenye ikulu.

Trump ataendelea kusimamia biashara zake akiwa Rais?

La hasha wakili wake amesema kuwa biashara zake Trump zitasimamiwa na watoto wake, Donald Junior, Ivanka na Eric.

Trump ataanza lini kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani?

Donald Trump alilifanya suala la ujenzi wa ukuta kwenye mpaka ili kuzuia wahamiaji haramu kuwa ajenda kuu wakati wa kampeni yake.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Ukuta utajengwa pahala pa ua huu?

Makala moja katika mtandao wake inaeleza jinsi atailazimisha Mexico kulipia gharama ya ujenzi wa ukuta huo

Kutoka na gharama kubwa inayohitajika na changamoto za kupata ardhi ya kuujenga ukuta , wadadisi wanasema kuwa ukuta huo huenda usijengwe. Kile wanachotarajia na kuboresha sera za mpaka na sheria za uhamiaji.

Atasitisha utoaji mimba?

Mwezi Machi Donald Trump alisema kwa utoaji mimba unahitaji kuharamishwa na aliunga mkono aina fulani ya adhabu kwa wanawake ambao hutoa mimba. Lakini baadaye alionekana kulegeza kamba akisema kuwa suala hio linastahili kushughulikiwa na majimbo binafsi.

Trump amesema kuwa anaunga mkono marufuku dhidi ya utoaji mimba, isipokuwa ile inayokana na ubakaji na wakati maisha ya mama yako hatarini.

Nina bima ya afya chini ya mfumo wa Obamacare. Nitaipoteza?

Donald Trump ametaja wazi kuwa kuondoa mfumo nafuu wa Obamacare ndio itakuwa ajenda yake kuu , na anarajia kuuondoa haraka iwezekanavyo.

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Anaweza kuamrisha shambulio la nyuklia?

Rais wa Marekani ana mamlaka ya kuamrisha shambulizi la nuklia mwa muda mfupi, mkoba wa nuklia au "football" jinsi unavyojulikana unawekwa karibu naye wakati wote, una namba ambazo atatumia kujitambulisha wakati anaamrisha makamannda kufanya shambulizi la nuklia.

Kisha inafuatia shughuli ya watu kadhaa na teknolojia ngumu ya kuchukua hatua ya kufanya shambulizi la nuklia.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Namba za siri za kufungulia silaha za nyuklia huwekwa kwenye mkoba ufahamikao kama "nuclear football"

Matamshi yake yamekuwa tofauti na ashasisitiza kwa kukosha utabiri ni muhimu wakati jeshi na mabomu nuklia hutumiwa

Ndoa za jinsia moja zitaendelea kutambuliwa?

Donald Trump amesema wakati wa mahojiano kuwa anapinga ndoa za jinsia moja licha ya yeye kudai kuwa ashahudhuria ndoa hiyo.

Chanzo cha picha, AFP

Amesema kuwa ni suala linalostahili kuamuliwa kwenye majimbo badala ya nchi nzima na alighadhabishwa na uamuzi wa mahakama mapema mwaka huu ambao ulihalalisha ndoa za jinsi moja kote nchini.

Lakini mapema mwaka huu alisema kuwa atawateua majaji wa mhakama ya juu kutupilia mbalia uamuzi huo.

Nini kitafanyika kwa kesi zake zilizo mahakamani?

Trump amehusishwa na kesi kadha ambazo ziko mahakania.

Kwa sasa Trump ana jumla ya kesi 75 zilizo mahakamani.

Kwa sahabu kesi hizo zilipelekwa mahakaman kabla aingie ofisini, Trump atahitajika kufika mahakamani kuhudhuria kesi hizo.

Mimi ni Mwislamu, bado nitaruhusiwa kuenda likizo nchini Marekani?

Baada ya ufyatuaji mkubwa wa risasi mwaka uliopita mjini San Bernardino ambapo watu 14 waliuawa, bwana Trump alitaka waislamu wote wazuiwe kuingia nchini Marekani.

Matamshi hayo yalikosolewa kote duniani na hata kutoka kwa mgombea mwenza Mike pence ambaye aliyataja kuwa yanayokiuka katiba.

Miezi kadha iliyopita Trump ameonekana kuachana na mipango hiyo.

Trump anaweza kubatilisha mikataba kuhusu mabadiliko ya tabia nchi?

Bw Trump haamini binadamu amechangia mabadiliko ya tabia nchi na anataka Marekani ijitoe Mkataba wa Paris.

Chanzo cha picha, PA

Hata hivyo Mkataba wa Paris tayari umetiwa saini na sasa ni sehemu ya sheria za kimataifa. Ingawa Trump anaweza kupata wanasiasa wa kumuunga mkono kuondoa Marekani kutoka kwa mkataba huo, shughuli ya kujiondoa rasmi inaweza kuchukua hadi miaka minne.

Trump atadhoofisha Nato na kuweka hatarini washirika wa Marekani?

Bw Trump amekuwa akisema washirika wa Marekani wanafaa kulipia ulinzi wanaopata kutoka kwa Marekani. Anataka kutathmini upya mchango wa Marekani katika shirika la kujihami la nchi za Magharibi, Nato.

Julai alisema iwapo nchi za Nato zitashambuliwa na Urusi, zinafaa kutarajia Marekani izisaidie iwapo zimekuwa zikitimiza masharti pekee.

Baada yake kushinda, baadhi ya viongozi wa Ulaya wamemtaka kufafanua. Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amemkumbusha kwamba mkataba huo hauna masharti.

Bado haijabainika iwapo ataweza kufikia maelewano na wanachama wa Nato.

Trump atashambulia Korea Kaskazini?

Mei, alisema anaweza kuketi na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kujaribu kuizuia Pyongyang isiendelee na mpango wake wa nyuklia, jambo ambalo ni tofauti na msimmao wa Marekani.

Alisema: "Ninaweza kuzungumza naye, sina tatizo kuzungumza naye."

Korea Kaskazini imemtaja kama "mwanasiasa mwenye busara" na wa "kuona mbali".

Korea Kaskazini imesema wazi kwamba haiko tayari kuacha kustawisha silaha za nyuklia.

Bw Trump amesema anaweza kuruhusu Japan na Korea Kusini anzo zistawishe silaha za nyuklia kama kinga dhidi ya Korea Kaskazini na Uchina.

Wamarekani watahamia sana Canada?

Baada ya ushindi wa Trumo, mtandao wa uhamiaji wa Canada ulipata hitilafu, watu wengi walipoutembelea labda kutaka kujua utaratibu wa kuhamia Marekani.

Ingawa ni rahisi Wamarekani kupata visa ya kwenda Canada, kuna masharti mengi iwapo mtu anataka kuhamia kabisa nchini humo.

Trump anaweza kuzuiwa kuzuru Uingereza?

Mwaka 2015 kulianzishwa ombi la "Block Donald J Trump from UK entry" (Mzuie Donald J Trump kuingia Marekani) kwa sababu ya matamshi ya uchochezi, baada yake kusema Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.

Ombi hilo lilipata saini zaidi ya nusu milioni na likajadiliwa bungeni Uingereza Januari 2016.

Ingawa ulijadiliwa, hakukupigwa kura yoyote hivyo hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa.