Marekani: Shambulizi liliwaua washirika Somalia

Map of Somalia

Shambulizi la angani nchini Somalia ambalo Marekani inasema kuwa lililenga wanamgambo wa al-Shabab liliwaua wanachama kumi wa kundi mshirika eneo hilo.

Marekani inasema iliendesha shambulizi hilo mwezi Septemba kulinda vikozi vya eneo la Puntland, ambavyo vilishambuliwa wakati wa oparesheni dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab.

Shambulizi hilo lilissbabisha kushuhudiwa maandamano ya kuipinga Marekanai kutoka kwa wenyeji.

Marekani hutoa msaada wa kijeshi kwa serikali ya Somalia wakati inapigana na wanamgambo wa al-Shabab.

Baada ya shambulizi hilo maafisa eneo la Galmadug waliulaumu utawala hasimu eneo al Puntland kwa kulipa jeshi la Marekani taarifa za uongo ili wafanye shambulizi lililowaua wanajeshi wake.

Puntland na Galmadug maenea ambayo yote yanajitawala yamekuwa yakipigana kwa miongo kadha kwa sababu ya mzoza wa mipaka.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Al-Shabab ni sehgemu la al Qaeda

Marekani imesema kuwa hakuna raia aliyeuawa wakati wa shambulizi hilo.