IS yauwa watu 40 na kuwaacha wakining'inia mjini Mosul

Oparesheni ya Mosul imeingia wiki ya nne Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Oparesheni ya Mosul imeingia wiki ya nne

Kundi la Islamic State liliwaua watu 40 siku ya Jumanne katika mji ulio Kaskazini mwa Iraq wa Mosul baada ya kuwalaumu kwa uhaini, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Miili yao iliachwa ikining'inia kutoka kwa vigingi vya umme kwenye wilaya kadha.

Mwanamme mmoja pia anaripotiwa kupigwa risasi hadharani kati kati mwa Mosul kwa kukaidi agizo la IS la kuwataka watu kutotumia simu ya mkoni.

Vikosi vya jeshi la Iraq vinaendelea na jitihada za kuteka mji wa Mosul kutoka kwa Islamic State.

Kuuawa kwa raia kunaonekana kutekelezwa kufuatia amri kutoka kwa mahakama zilizobuniwa.

Umoja wa mataifa pia unasema kuwa raia 20 waliuwa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano jioni kwenye kambi ya kijeshi ya Ghabat Kaskazini mwa Mosula kwa madai ya kufichua habari.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nyumba iliyotumiwa na IS ilitekwa na vikosi vya Iraq Mashariki mwa Mosul

Umoja wa Mataifa pia umeelezea hofu ya IS kuwaajiri kama wapiganaji watoto wadogo wa kiume.

Islamic State pia ilitangaza mnano tarehe 6 mwezi huu kuwa iliwakata vichwa wanamgambo saba waliokimbia eneo la vita katika wilaya ya Kokjali Mashariki mwa Mosul.

Image caption Vikosi vya serikali vilianzisha mapigano ya kuuteka mji wa Mosul mwezi uliopita.

Vikosi vya serikali vilianzisha mapigano ya kuuteka mji wa Mosul mwezi uliopita. Mji huo umekuwa umedhibitiwa na Isamic State tangu mwaka 2014.

Kwa sasa oparesheni hiyo imeingia wiki yake ya nne na inawajumuisha vikosi vya usalama 50,000 vya Iraq, polisi, wapiganaji wa kurdi, wasunni na wapiganaji wa Shia.