Watu 11,000 wamekamatwa nchini Ethiopia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makabila ya Oromo na Amhara yamekuwa yakiandamana nchini Nigeria

Takriban watu 11,000 wamekamatwa kutokana na uhalifu unaohusiana na hali ya hatari iliyotangazwa nchini Ethiopia, na maandamano yenye ghasia kwa mujibu wa bodi iliyoteuliwa na serikali.

Bado haijabainika ikiwa watu hao wote bado wako kizuizizi au ikiwa baadhi yao wameachiliwa.

Mwezi Oktoba serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya hatari ya miezi sita kufuatia maandamano yaliyoshuhudiwa kutoka kwa makabila makubwa zaidi nchini humo.

Makabila ya Oromo na Amhara huchukua asilimia 60 ya watu wote. Wengi wao hulalamika kuwa mamlaka yamedhibitwa na kabila dogo la Tigrean.