Kambi ya jeshi la Marekani yashambuliwa Afghanistan

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bagram mara nyingi imelengwa na Taliban

Kumeripotiwa shambulizi kubwa lililofanywa na wanamgambo kwenye kambi kubwa zaidi ya wanajeshi wa Marekani ya Bagram nchini Afghanistan.

Jeshi linaloongozwa na NATO, lilisema kuwa watu wanne waliuawa na hadi 14 kuejruhiwa wakati kifaa kimoja kililipuliwa.

Maafisa wanasema kwa huenda mlipuaji alikuwa ni mshambuliaji wa kujitoa mhanga, ambaye alidanganya kuwa mfanyakazi wakati wafanyakazi walikuwa wakiwasili katika kambi hiyo kwa shughuli za siku.

Kundi la Taliban linasema kuwa ndilo lilihusika. Hakuna taarifa zaidi kuhusu uraia wa wale waliouawa.