Ujumbe wa wafu waonekana kimakosa kwa watumiaji wa Facebook

Haki miliki ya picha facebook
Image caption Ujumbe huo ulionekana kwenye ukurasa wa mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg

Ujumbe usio wa kawaida katika mtandao wa Facebook kimakosa umeonyesha kuwa watu wengi walikuwa wamekufa.

Tatizo hilo lililotokea siku ya Ijumaa lilisababisha mtandao wa Facebook kuonyesha bango la wafu kwa kurasa za watu ambao tayari walikuwa hai.

Watumiaji wa mtandao walilazimika kundika tena kuwahakikishia marafiki na familia zao kuwa bado walikuwa hai.

" Hili lilikuwa ni tatizo kubwa na sasa tumelitatua" msemaji wa Facebook alisema." Tunaomba msamaha kwa kile kilichotokea.

Ujumbe huo ulionuiwa kutumiwa kwa kurasa za watu waliokuwa wamekufa, ulionekana kwa watumiaji wengi wa Facebook ukiwemo ukurasa wa mkurugenzi mkuu Mark Zuckerberg.

Ujumbe huo ulianza kutumiwa kwenye mtandao wa Facebook mwaka 2015, baada kesi ambapo familia zilitaka kutumia akaunti za wapendwa wao waliokuwa wamekufa.