Mamia ya wahamiaji waokolewa katika bahari ya Mediterranean

Image caption Maelfu ya wahamiaji hujaribu kufanya safari hatari, ya kuvuka kutoka Afrika Kaskazini kuelekea Ulaya

Shirika linalofanya uokozi katika Bahari ya Mediterranean, linasema linajaribu kuwaokoa wahamiaji kama 700 wanaoelea kwenye mashua baharini.

Shirika hilo linalofahamika kama Migrant Offshore Aid Station, linasema lilianza kazi hiyo leo alfajiri.

Maelfu ya wahamiaji kila juma, wanajaribu kufanya safari hiyo ya hatari, ya kuvuka kutoka Afrika Kaskazini kuelekea bara la Ulaya, ingawa hali ya hewa inazidi kuwa mbaya huko majira ya baridi yakikaribia.

Umoja wa Mataifa unasema, katika mwaka huu, tayari wahamiaji wengi kabisa wamekufa maji katika Mediterranean. Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 4000 wamezama tangu mwaka kuanza.

Mada zinazohusiana