UN katika jitihada za kutatua mzozo wa kisiasa DRC

Kuna madai kuwa Kabila anachelewesha uchaguzi ili abaki madarakani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuna madai kuwa Kabila anachelewesha uchaguzi ili abaki madarakani

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wanazuru Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kujaribu kuzima mvutano wa kisiasa nchini humo.

Rais Joseph Kabila anamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho mwezi ujao, lakini uchaguzi umehairishwa.

Upinzani unamtuhumu rais kwamba anachelewesha uchaguzi makusudi ili abaki madarakani.

Shirika la kutetea haki za binaadamu, Human Rights Watch, limeliomba Baraza la Usalama kumsihi Rais Kabila aondoke madarakani muhula wake ukimalizika, ili kuepusha msukosuko mkubwa zaidi.