Serikali ya Syria yatwaa maeneo ya Aleppo kutoka kwa waasi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mji wa Aleppo umekuwa kwenye vita tangu mwaka 2012

Waangalizi wa mzozo ulio nchini Syria wanasema kuwa vikosi vya serikali vimetwaa maeneo yoye ya mji wa Aleppo ambayo yalitekwa na wapiganaji waasi wiki mbili zilizopita.

Waangalizi hao kutoka shirika la (Syrian Observatory for Human Rights), walisema kuwa wanajeshi hao walikuwa wamechukua udhibiti wa mkoa ulio magharibi wa Dahiyet al-Assad na kijiji cha Minyan kilicho nje ya mji wa Aleppo.

Waasi walifanya mashambulizi mwishoni mwa mwezi Oktoba, katika jitihada za kutaka kupenya maeneoa yaliyokuwa yamezingirwa mwezi Julai sehemu wanazodhibiti mashariki mwa mji wa Aleppo.

Mada zinazohusiana