Watu 30 wauawa kwenye shambulizi Pakistan

Image caption Shambulizi lilitokea kwenye madhabahu yaliyo mkoa wa Balochistan

Takriban watu 30 wameuawa kwenye shambulizi lililotokea kwenye madhabahu ya kiislamu yaliyo mkoa wa Balochistan, kwa mujibu wa maafisa nchini Pakistan.

Watu wengine kadha wanaripotiwa kujeruhiwa katika madhabua ya Shah Noorani yaliyo wilaya ya Kunduz.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa hakuna hospitali iliyo karibu na watoa huduma za dharura wanajaribu kufika eneo hilo kwa sababu liko mbali.

Waliojeruhiwa wanaripotiwa kusafirishwa kwenda Karachi, pwani ya Pakistan kuweza kupata matibabu.

Mwezi Oktoba watu kadha waliuawa kwenye shambulizi lililotokea katika taasisi ya kutoa mafunzo kwa polisi, iliyo mji wa Quetta.

Shambulizi lingine lililofanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga liliwau watu 70 kwenye hospitali mjini Quetat mwezi Agosti.