Iraq yaukomboa mji wa Nimrud kutoka kwa IS

Wanajeshi wa Iraq waukombia mji wa zamani wa Nimrud Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Iraq waukombia mji wa zamani wa Nimrud

Jeshi la iraq linasema kuwa limeukomboa mji wa zamani wa Nimrud kutoka wapiganaji wa Islamic State.Mji huo upo yapata kilomita 30 kutoka mji muhimu wa Mosul ,ambao jeshi la Iraq linajiribu kuuteka kutoka kwa wapiganaji wa IS.

Wapiganaji hao wamefanya uharibifu mkubwa mjini Nimrud ,uliogunduliwa katika karne ya 13 kabla ya kujiri kwa Yesu.

IS wanasema kuwa makaburi na masanamu hayafai na ni lazima yaharibiwe.

Taarifa ya jeshi la Iraq inasema kuwa vikosi kutoka kwa jeshi la tisa viliukomboa mji huo na kuweka bendera ya Iraq juu majumba yake baada ya kusababisha mauaji mengi na uharibifu wa vifaa vya wapiganaji hao wa Islamic State.