Rais wa Korea Kusini achunguzwa

Rais Park Guen Hye Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Park Guen Hye

Taarifa za vyombo vya habari nchini Korea Kusini zinasema waendesha mashtaka wanahoji uhusiano kati ya baadhi ya viongozi wa makampuni makubwa nchini humo, Rais Park Guen Hye na mwanamke anayetuhumiwa kutumia wadhifa wa rais huyo kujinufaisha kifedha.

Mwenyekiti wa kampuni ya kuunda magari ya Hyundai na mkurugenzi wa kampuni kubwa ya kutengeza vyuma nchini humo POSCO ni miongoni mwa wale wanaochunguzwa.

Waendesha Mashtaka pia wana mpango wa kumhoji mwenyekiti wa kampuni ya Sumsang

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano dhidi ya rais nchini Korea Kusini

Tayari mwanamke Choi Soon-sil amekamatwa na kushtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma na utumizi mbaya wa mamlaka.

Hapo jana maelfu ya raia waliandamana katika mji mkuu wa Seoul kumtaka Rais Park Guen Hye Kujiuzulu.