Aliyeongoza Brexit akutana na Donald Trump

Donald Trump na mtu aliyeongoza vuguvugu la Brexit Nigel farage wakutana
Image caption Donald Trump na mtu aliyeongoza vuguvugu la Brexit Nigel farage wakutana

Nigel Farage mtu mashuhuri ambaye aliongoza vuguvugu la Brexit na kufanikiwa kuiondoa Uingereza kutoka Muungano wa Ulaya ni mwanasiasa wa kwanza wa taifa hilo kukutana na Donald Trump tangu achaguliwe kuwa rais wa Marekani.

Viongizi hao walikutana katika Jumba la Trump mjini New York.

Msemaji wa Bw. Trump amesema mazungumzo kati yao yaliangazia uhuru na ushindi.

Nigel Farage amesema Trump ana mawazo ya busara na kwamba atakuwa Rais mzuri.

Wakati wa kampeini za uchaguzi wa Urais wa Marekani,Farage aliwahi kumpigia debe Bw Trump na kufananisha kampeni yake na vuguvugu la Brexit.