Kenya: Hatutashirikiana na UN Sudan Kusini

Wanajeshi wa Kenya waliopo nchini Sudan Kusini wametakiwa kurudi nyumbani
Image caption Wanajeshi wa Kenya waliopo nchini Sudan Kusini wametakiwa kurudi nyumbani

Serikai ya Kenya inasema kuwa iko tayari kulisaidia taifa la Sudan Kusini kuimarisha uthabiti wake lakini sio kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNMISS.

Kenya iliondo vikosi vyake kutoka nchini Sudan Kusini kufuatia kupigwa kalamu kwa kamanda wake na Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.

Akizungumza katika ikulu ya Whitehouse jijini Nairobi,msemaji wa serikali Manoah Esipisu amesema kuwa Kenya itashirikiana na Sudan Kusini kupitia mashirika lakini haitasitisha msimamo wake wa kuondoa wanajeshi wake walinda amani.

Bw Esipisu ,amesema kuwa hatua ya UNMISS kushindwa kuishauri Kenya kuhusu hatua yake ya kumfuta kazi kamanda wake Luteni jenerali Johnson Ondieki inaonyesha ukosefu wa heshima kwa Kenya.

Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Mamia ya wanajeshi wa Kenya waliokuwa wakihudumu nchini Sudan Kusini katika jimbo la Wau tayari wamewasili mjini Nairobi.

Wanajeshi zaidi wanatarajiwa kuwasili katika majuma kadhaa yajayo kufuatia hatua ya rais Uhuru Kenyatta ya kuwataka warudi nyumbani.

Viongozi wa upinzani nchini Kenya wameikosoa serikali kwa kuchukua hatua hiyo.