Taifa Stars yachapwa 3-0 na Zimbabwe

Michezo Haki miliki ya picha Google
Image caption Taifa Stars na Zambia wakimenyana

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imechapwa ugenini na Zimbabwe kwa mabao 3-0 na katika mchezo wa kirafiki.

Mshambuliaji wa Zimbabwe Knowledge Musona ndie alianza kuiandikia timu yake bao la kwanza dakika ya tisa kabla ya mshambuliaji Matthew Rusike kuongeza bao la pili.

Msumari wa mwisho wa Zimbabwe uliwekwa kambani na Nyasha Mushekwi katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili.Safu ya ushambuliaji ya Tanzania ikiongozwa na Mbwana Ally Samatta alidhibitiwa vikali sawa na kushindwa kufurukuta.