Mwezi mkubwa zaidi kuonekana duniani

Mwezi mkubwa zaidi kuonekana Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwezi mkubwa zaidi kuonekana

Watazamaji wa anga wanajiandaa kuuona mwezi mkubwa zaidi wakati ambapo utakaribia dunia tangu 1948.

Uingereza itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi huo siku ya Jumatatu jioni,licha ya kuwa utakaribia dunia mwendo wa saa tano na dakika 21 muda wa GMT ambapo utakuwa umbali wa kilomita 356,509.

Wachunguzi watauona mwezi huo kuwa mkubwa zaidi kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwezi wa kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15, licha ya kwamba macho ya binaadamu yanaweza kupambanua tofauti hiyo.

Huku mwezi huo ukitarajiwa kutokaribia dunia hadi tarehe 25 mwezi Novemva 2034, idara ya maswala ya hewa nchini Uingereza imesema kuwa kutakuwa na mawingu mazito wakati mwezi huo utakapokaribia.

Huku mwezi ukizunguka dunia,kuna tofauti ya mwangaza unaotolewa na jua.Ni wakati huo ambapo mwezi wote humulikwa na mwangaza huo na kutoa mwezi mkubwa zaidi.