Tetemeko la pili lakumba kisiwa cha New Zealand

Athari za tetemeko la ardhi nchini New Zealand Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Athari za tetemeko la ardhi nchini New Zealand

Tetemeko la pili la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika vipimo vya Ritcher limekumba kisiwa cha kusini mwa New Zealand ,saa chache tu baada tetemeko jingine kubwa kupiga kisiwa hicho na kuwaua watu wawili.

Tetemeko hilo lilipiga mwendo wa saa saba na dakika 45 mchana katika kina cha kilomita 10,kaskazini mashariki mwa mji wa Christ Church.

Tetemeko lenya ukubwa wa 7.5 lilikuwa limekumba eneo hilo awali mda mfupi baada ya saa sita usiku na kusababisha onyo la Tsunami.

Mto mkubwa uliofurika umevunja kingo zake na kusababisha mafuriko katika maneo ya chini.

Wakaazi karibu na mto Clarence,ambao ni mkubwa katika kisiwa hicho cha kusini walikuwa wakiagizwa kuhamia maeneo ya juu.