Mwaka 2016 'una uwezo' wa kuvunja rekodi ya mwaka wenye joto zaidi ulimwenguni

mifungo iliyokufa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mifugo iliokufa kutokana na kiangazi

Mwaka 2016 unadhaniwa kuwa mwaka wenye joto zaidi ulimweguni,kulingana na data za hapo awali.

Kutokana na data ya miezi tisa ya kwanza , wanasayansi wanahakika kwa asilima 90 joto litapita kiwango cha alama kilichowekwa mwaka wa 2015.

Viwango vya joto kutoka Januari hadi Septemba vilikuwa nyuzi 1.2 zaidi ya kiwango kinachotoka kwa viwanda kulingana na shirika la kimataifa ya maswala ya hali anga (WMO).

Shirika hilo limesema viwango vya joto vinastahili kusalia katika kiwango cha juu kwa siku zilizosalia ili kuvunja rekodi ya mwaka jana.

El Nino imekuwa na athari zake, lakini kile kinachosababisha kiwango cha joto kuzidi kuongezeka ni utoaji wa gesi chafu ya kaboni.

Uchaguzi wa Donald Trump kama rais wa Marekani umeongeza matarajio ya kwamba atakuwa na maoni tofauti kuhusiana na maswala ya mabadiliko ya hali anga.

Wanasayansi wanasisitiza kwamba swala la mabadiliko ya hali ya anga linazidi kuongezeka kila mara.

Mwaka wa 1998 ndio mwaka pekee ambao haukushuhudia kiwango kikubwa cha joto ulimwenguni.