Watu 10 wauawa kwenye ghasia Nigeria

Waislamu wa madhehebu ya Shia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waislamu wa madhehebu ya Shia

Takriban watu kumi sasa wanafahamika kuuawa Kaskazini mwa Nigeria, kufuatia ghasi kati ya vikosi vya usalama na waislamu wa madhehebu ya Shia kwenye mji wa Kano.

Polisi wanasema kuwa ghasia zilizuka wakati waislamu wa Shia waliokuwa wakielekea kwenye mkutano wa kidini waliposhambuliwa kwa silaha zikiwemo panga na mishale.

Watu hao waliripotiwa kunyakua bunduki ya polisi ambayo kwa sasa imepatikana.

Hata hivyo washia hao wanapinga madai hayo wakisema kuwa polisi waliwashambulia wakati walikuwa wakiandamana kwa amani.

Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran lina historia ya mzozo wa mipaka na vikosi vya usalama.