Lampard: Kuiaga klabu ya New York City

Frank Lampard Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Frank Lampard

Kiungo wa kati wa zamani wa England na Chelsea, Frank Lampard amesema ataiaga ligi ya MLS ya New York City.

Lampard mwenye umri wa miaka ,38, ambaye mkataba wake utakamilika mwishoni mwa mwaka huu , amechapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba wakati wake katika klabu hiyo ''umefika kikomo.''

Amesema atatangaza hadharani ' hatma yake ya siku zijazo' hivi karibuni.''

Lampard amefunga mabao 15 katika mechi 31 alizoshiriki katika klabu ya New York ,kwa miaka miwili iliyokatizwa na mkopo kutoka Manchester City.

New York City walifungwa mabao 7 kwa nunge na klabu ya Toronto FC katika hatua za kwanza za mwezi.

Lampard alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2014, na kuvunja rekodi ya mabao 211.

Mwenzake wa timu ya timu ya Uingereza na Liverpool Steven Gerrard pia anaweza kumaliza muda wake nchini Marekani

Gerrard, 36, amesema amekamilisha mkataba wake kwa akiichezea klabu ya LA Galaxy na amesema anaweza kuhudumu kama mkufunzi kwa klabu yake ya Liverpool.