Uchunguzi kuhusu habari potovu kwenye Facebook waendelea

Zuckerberg Haki miliki ya picha AP
Image caption Mark Zuckerberg

Licha ya juhudi za Mark Zuckerberg kukana kwamba mtandao wa facebook ulimsadia Donald Trump, uchaguzi jinsi habari potuvu zinavyosambaa katika mtandao huo unaendelea.

Habari za Buzzfeed zinaripoti kuwa zaidi ya watu kumi na wawili ambao ni waajiriwa wa facebook wameungana kubuni kikosi maalumu ili ushugulikia swala hilo.

Buzzfeed, imemnukuu mmoja wa kikosi hicho kilichoteuliwa , ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutokana na hofu ya kazi yake.

"Mark Zuckerberg anafahamu, na wengine wetu katika kampuni twajua, kuhusiana na habari potovu katika mtandao huo katika msimu wa kampeini ,'' mfanyikazi mmoja amesema.

Facebook haijajibu ombi la BBC kuhusiana na ripoti hiyo ya Buzzfeed.

Google siku ya Jumatatu ilitangaza itaongeza jitihada za kukabiliana na mitandao bandia kupata pesa kutoka kwa matangazo.

Muda mfupi baadaye Facebook walifanya tangazo sawa na la Google kwa matumizi ya mtandao wao wa matangazo.